Monday, 3 December 2007

Kaka mchezaji bora Ulaya


Paris, Ufaransa
MCHEZAJI nyota wa AC Milan , Ricardo Kaka ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya wa mwaka 2007, huku Cristiano Ronaldo wa Manchester United akiwa wa pili. Mchezaji huyo wa Brazili mwenye umri wa miaka 25, alikuwa mfungaji bora kwa kufunga magoli 10 katika ligi ya Mabingwa Ulay, huku timu yake ikitwaa taji hilo kwa kuifunga Liverpool mabao 2-1 katika fainali iliyofanyika Athens, Ugiriki. Ameshinda mpira wa dhahabu baada ya kupata alama za juu 444 katika kura zilizipigwa na kukusanywa na jarida la France Football kutoka kwa waandishi 96 wa sehemu mbalimbali duaniani. Kila mmoja alitakiwa kuwapigia kura wachezaji 50 na Ronaldo ameshika nafasi ya pili kwakupata alama 277.
kessy58..................................................

No comments: