Thursday 28 May 2009

Barcelona yachukua ubingwa wa Ulaya mbele ya Manchester United.

Shangwe ,vigelegele vikitawala kwa wanaume wa shoka Barca.
Manchester wakibaki na butwaa baada ya kupokonywa kombe na Barca.

C.Ronaldo haamini macho yake.


Messi akishangilia goli lake.



Samuel eto'o akishangilia goli lake la ufunguzi.

Barcelona ndio mabingwa wa kombe la klabu bingwa ulaya kwa kuitandika bila huruma Manchester Unitetedkwa magoli 2-0 huko Rome Itali.Mabao ya eto'o na Messi ndio yaliyokata kidomodomo cha mashetani hao wekundukama wangeshinda ingekuwa kelele mtindo mmoja.
kessy58......................................................................


Wednesday 27 May 2009

Klabu bingwa ulaya leo,Barcelona na Manchester United.







LEO ndiyo leo. Baada ya kelele, majigambo na tambo za kila aina Barcelona ya Hispania na Manchester United ya Uingereza, zinaumana usiku huu katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.Mechi hiyo inayokutanisha mafahari wawili na timu maarufu duniani itapigwa kuanzia saa 2:45, usiku kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini hapa.Katika mechi hiyo, Man United inapigania kutwaa kombe hilo kwa mara ya nne na pia ikitaka kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza Ulaya kutetea taji hilo.Barceloma 'Barca' wao wanataka kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu angalau kupunguza tofauti yao na wapinzani wao wa jadi, Real Madrid ya Hispania iliyotwaa kombe hilo mara tisa.Klabu zingine zilizotwaa kombe hilo mara nyingi ni Liverpool ya Uingereza na AC Milan ya Italia mara 5 kila moja.United "Mashetani Wekundu" wanakutana na Barcelona fainali ya kwanza katika historia ya klabu hizo maarufu duniani.Zote zinaingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu zilizo sawa kwa kila moja kutwaa ubingwa katika Ligi Kuu ya nchi yake msimu huu unaomalizika. Barcelona iliingia fainali kwa kunufaika na goli la ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Chelsea ya Uingereza katika mchezo wa marudiano jijini London baada ya kutoka suluhu mechi ya awali Barcelona.Kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson ambaye anapigania taji la 26 katika misimu 23 ya kuwaongoza Mashetani Wekundu anasema kwamba pambano hilo litakuwa la kuvutia."Uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili wanaonesha ni kiwango gani cha mpira kitaoneshwa," alisema Ferguson.Lakini, Ferguson atakuwa na kazi nzito ya kuwaandaa mabeki wke kuikabili safu kali ya ushambuliaji ya Barca ya Thierry Henry, Lionel Messi na Samuel Eto”o ambayo msimu huu imefunga magoli 100.Lakini naye Ferguson ana safu nzuri ya ushambuliaji inayoundwa na Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney, Dimitar Berbatov na Carlos Tevez.
kessy58............................................................



Tuesday 5 May 2009

Hukumu ya nusu fainali klabu bingwa ulaya leo.

Timu za Arsenal na Manchester United zinajimwaga tena leo uwanjani katika kinyang'anyiro cha nusu fainali klabu bingwa ulaya.
kessy58........................................................

Tuesday 28 April 2009

leo ndio leo klabu bingwa ulaya


Barcelona 20:45 Chelsea
kessy58...................................................................

Thursday 16 April 2009

Arsenal na Manchester zatinga nusu fainali klabu bingwa ulaya




Timu ya Arsenal jana imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la klabu bingwa ulaya baada ya kuinyuka timu ya Villarreal jumla ya magoli 3-0.Nao mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester united imefanikiwa kuingia nusu fainali kwa kuinyuka timu ya FC porto kwa goli 1-0.Kwa matokeo hayo timu ya Arsenal na Manchester watakutana katika nusu fainali tarehe 29/-04/2009.
kessy58..................................................................



Wednesday 15 April 2009

Chelsea na Brcelona zapepeta,Arsenal-Villarreal,Manchester-FC porto dimbani leo


Timu ya chelsea imetinga nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa ulaya baada ya kutoka sare ya magoli 4-4 na Liverpool.Nao vinara wa Spain fc Barcelona imetinga nusu fainal ya mashindano hayo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Bayern Munich.kwa matokea hayo timu ya Barcelona na Chelsea watachuana vikali katika nusu fainali.
Mtanange wa mashindano hayo unaendelea tena leo kwa kuzikutanisha timu kati ya Arsenal na Villarreal,FC porto na Manchester United.
kessy58...............................................................


Wednesday 8 April 2009

Klabu bingwa ulaya Manchester,Villarreal taabani




Timu ya Manchester United jana imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya magoli 2-2 na timu ya porto katika kinyang'anyiro cha klabu bingwa bingwa.Nao vijana wa Arsenal wameilzamisha sare ya goli 1-1 dhidi ya wenyeji wao Villarreal.Villareal ndio iliyokuwa ya kwanza kuona nyavu za Arsenal katika dakika 10 kupitia kwa M. Senna,Arsenal nao walicharuka zaidi kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha goli katika dakika ya 66 lilifungwa na E.S. Adebayor.Mtanange wa mashindano hayo unaendelea tena kwa kuzikutanisha timu ya Barcelona na Bayern Munich,Liverpool naChelsea.
kessy58.....................................................................