Jibu la swali hilo litapatikana mjini Moscow, Urusi katika uwanja wa Luzhniki baada ya kumalizika dakika 90 au 120 katika mechi ya fainalia itakayokutanisha timu hizo ambazo zilikuwa zikichuna katika Ligi ya Uingereza kabla ya Manchester United kuibuka mabingwa.
Hii ni fainali ya kwanza kuzikutanisha timu za Uingereza tupu.Wakati Chelsea inayonolewa na kocha Avrem Grant imefuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza katika historia yake, United inataka kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu baada ya kutwaa mara ya mwisho mwaka 1999 mjini Barcelona Hispania kwa kuifunga Buyern Munich mabao 2-1 katika dakika mbili za mwisho.
Jana na leo ndege ziliongeza safari kati ya Uingereza na Moscow kubeba mashabiki kiasi cha 40,000 wa timu hizo wanaotaka kushuhudia fainali hiyo. Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) Michel Platini amesema fainali hiyo itafanyika kwa usalama na kila kitu kimewekwa sawa.
United leo inatarajiwa kupanga kikosi chake mchanganyiko chenye wachezaji wakongwe na chipikizi. Ryan Giggs, ambaye alikuwemo kwenye fainali ya 1999, anaweza kucheza leo na kuvunja rekodi ya kucheza mechi nyingi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton katika klabu hiyo kwa kucheza mechi 758.
Chelsea baada ya kukosa ubingwa wa Uingereza kwa United leo itatolea macho fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya ili kuweka kumbukumbu ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza. Inatarajiwa kuwa na wachezaji wake walinzi Ricardo Carvalho na John Terry na mshambuliaji Didier Drogba.
Kocha Avram Grant anaweza kumtumia mchezaji mmoja kati ya Florent Malouda au Salomon Kalou katika sehemu ya kushoto. Wengine wanaoweza kuwemo ni Ashley Cole na kiungo Michael Essien, Claude Makelele.
Mara ya mwisho timu hizo zilipambana katika Ligi Kuu na Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Stamford Bridge.
kessy58...................................................................................

No comments:
Post a Comment