Binti abakwa, kisha abakwa tena Polisi
Maskini binti wa watu aliyefikishwa kituo cha Polisi baada ya kubakwa, amebakwa tena na Askari Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Tayari Polisi huyo amesimamishwa kazi, tukio lililothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kusini Unguja, Khamis Ramadhan na uchunguzi unaendelea ili afikishwe mahakamani.
Binti huyo alifikishwa kituoni hapo na wenzake baada ya kubakwa na watu wasiojulikana wakati wakitafuta kuni katika Msitu wa Pongwe
Siku ya mkasa huo mabinti hao waliondoka makwao mida ya saa 11:00 jioni na hawakurejea hadi wazazi waliopowatafuta na walipowapata ndio wakaeleza mkasa uliowapata.
Kamanda Ramadhan alisema kuwa wazazi hao waliamua kuwapeleka kituo cha Chwaka ili uchunguzi wa kuwasaka wahusika katika msitu huo uanze mara moja.
Baadhi ya askari waliondoka kituoni hapo kwenda kuwasaka wabakaji hao na ndipo askari aliyebaka na mabinti hao kituoni alimvamia mmojawao na kumbaka.
Tukio hilo limewapakazia jeshi la Polisi wa kituo hicho na kuibua mtafaruku mkubwa na wananchi wa eneo hilo hadi Mkuu wa Wilaya Ali Hassan Khamis alipotinga kituoni hapo na kutuliza hali hiyo.

No comments:
Post a Comment