London,Uingereza.
KOCHA wa zamani wa Chelsea ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wanaofaa kukinoa kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza, Jose Mourinho, imebainika kuwa ameanza kufanya mazungumzo ya siri na maofisa wa Chama ch.a Soka cha hapa (FA).
Katika mazungumzo hayo ya siri Mourinho ambaye awali alisema hana mpango wa kurejea Uingereza, sasa ameshatamka ramsi: Nataka kuinoa Uingereza."Habari zinasema kuwa makubaliano yanakwenda vizuri na tayari bosi wa FA, Brian Barwick amekubali kumpa kocha huyo kitita cha pauni milioni sita kwa mwaka.
Vyanzo vya kuaminika vimekaririwa na gazeti la The Sun la Uingereza toleo la jana kuwa Mourinho,44, alisafiri kwa ndege maalum ya kukodi huku safari yake ikigubikwa na usiri mkubwa na kufika mjini London anakotarajiwa kokutana na viongozi wa FA.
Ndege hiyo iliyomchukua kocha huyo ambaye amekuwa akitajwa na mashabiki wengi wa soka kuwa anafaa kupewa timu hiyo inayohitaji kocha mhamasishaji, ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Farnborough airport, Hants.
Morinho ilielezwa kuwa awali alipanga kutua kwenye uwanja huo siku moja kabla lakini akabadili ratiba kuepuka kuonekana na wanahabari. Uwanja huo hutumiwa na mastaa wengi akiwemo David Beckham na Elton John kwa safari zao za siri.Kurejea England kwa Mourinho kunaelezwa kuwa kumechangiwa pia na msimamo wa mkewe, Tami, 41, ambaye anaelezwa kuwa alishayazoea maisha ya London. Pia watoto wa kocha huyo, Matilde,10 na Jose Jr, 6, nao walikuwa wakipenda kurejea mjini humo.
Chanzo kilicho karibu za Mourinho kililiambia The Sun kuwa: “ Hakuna shaka kuwa Jose sasa anaitaka kazi ya ukocha wa England kwa nguvu zote. Yeye ni chaguo namba moja la FA kwa sasa. Cha msingi kwa ni Jose kupitia vipengele vya mkataba.
Ndio maana amesafiri kwenda London kuonana na Barwick na maofisa wengine wa Bodi ya FA. Suala hapa ni utayari wa FA kumpatia kitita atakachokitaka.”Chanzo hicho kiliongeza: “Familia ya Jose inapenda kuishi Uingereza na yeye yuko tayari kuwatimizia hilo"The Sun lilipomtafuta kwa njia ya simu na kumuuliza Barwick juu ya ujio huo wa Mourinho alikaa kimya kwanza kabla ya kusema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa.
Mashabiki wengi wa England wamekuwa wakitaka Mourinho kocha aliyepata kujiita 'Mtu Maalum' apewe nafasi hiyo ili kuwarejeshea wachezaji wa nchi hiyo ari ya kimchezo baada ya kushindwa kufuzu michuano ya Euro mwakani.
kessy58............................................................

No comments:
Post a Comment