Saturday, 19 January 2008

Adebayor mwanasoka bora afrika


Tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika itolewayo na BBC kwa mwaka wa 2007 imekwenda kwa mshambuliaji machachari wa klabu ya Arsenal, Emmanuel Adebayor wa Togo.
Mshambuliaji huyo alipata zaidi ya asilimia 40 ya kura zote na kumshinda Didier Drogba wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea ambae aliishia nafasi ya pili.
Adebayor aliiambia BBC kwamba amefurahi kupata tuzo hiyo kubwa.
''Ushindi wangu una maana kubwa. Kushinda ni vizuri lakini ni bora zaidi iwapo unamaanisha mabadiliko makubwa katika maisha ya wale waliokosa fursa, ningependa kuwa wakala wa mabadiliko katika maisha ya mamilioni ya vijana wa kiafrika ambao wamepoteza matumaini''.
''Watoto kama hawa ndio viongozi watarajiwa wa kesho na lazima wapewe msaada ili kuwapa nguvu wawe raia makini wa Afrika'' alisema Adebayor.
Adebayor anasema ushindi wake una maana kubwa
Mchezaji wa kiungo wa Ghana, Michael Essien ambae alitwaa tuzo hiyo mwaka jana aliambulia nafasi ya tatu.
Mchezaji wa bora wa Afrika ni tuzo inayotolewa na idhaa ya Ulimwengu ya BBC na mshindi hupatikana kutokana na kura za wasikilizai na wasomaji wa mtandaoni.
Waliowahi kushinda tuzo hiyo miaka ya nyuma ni Sammy Kuffour,
Mohamad Barakat wa Misri, El Hadj Diouf wa Senegal na mnigeria Jay Jay Okocha.
kessy58......................................................................

No comments: