KITENDAWILI cha nani kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza huenda leo kikawekwa bayana wakati miamba mitatu inayowania ubingwa huo, Manchester United itakaposhuka dimbani kumenyana na Liverpool mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford huku Chelsea ikiwakaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Manchester United ambayo Jumatano wiki hii iliitungua Bolton Wanderers, ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa imevuna pointi 70 kutoka katika mechi 30 ilizocheza katika ligi hiyo. Arsenal, ambao wametoka sare katika mechi zake nne za mwisho, inayoshikilia nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 katika mechi 30 ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 65 baada ya kuongoza kwa magoli 3-1 na kisha kujikuta ikilazimishwa sare ya bao 4-4 na Tottenham Hotspur katika mechi iliyochezwa Jumatano wiki hii.
Liverpool imeshinda mechi zake tano za mwisho inashikilia nafasi ya nne, wao wanaonekana kutokuwemo katika kinyanganyiro hicho kutokana na kuwa na pointi 59 katika mechi 30 . Hata hivyo, endapo timu hiyo ikaibuka na ushindi kwenye Uwanja wa Old Trafford kunaweza kuweka hai matumaini yao ya kunyakua ubingwa.
Manchester United ambao wameshinda mechi zake nne tangu walipoangukiwa na Manchester City, wanatabiriwa kuibuka na ushindi wa pili dhidi ya Liverpool baada ya kuichapa timu hiyo bao 1-0 katika mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Anfield Desemba mwaka jana.
kessy58......................................................................................................

No comments:
Post a Comment