Monday, 24 March 2008

Liverpool,Arsenal aibu tupu


Timu ya liverpool jana ili kufurukata ndani ya old traford baada ya kukandamizwa magoli 3-0 na Manchester United,goli la manchester lilipatikana kipindi cha kwanza kutoka kwa mchezaji wao Wes Brown.dakika mbili kabla ya mapumziko mchezaji J. Mascherano wa liverpool alilambwa kadi nyekundu,goli la pili na la tatu la manchester yalipatikana katika kipindi cha pili kupitia wa wachezaji C. Ronaldo na Nani,kwa matokeo hayo yameifanya machester kuzidi kushika usukani kwa point 73.Nao vijana wa emirate wamesidi kuporomoka toka nafasi ya kwanza mpaka ya tatu baada ya kulambwa magoli 2-1 na timu ya chelsea,arsenal ndio ilikuwa ya kwanza kuona lango la wenyeweji chelsea katika dakika ya 59 kupitia kwa mchezaji B. Sagna,mnamo dakika ya 73 D. Drogba aliwainua vijana wa chelsea kwa goli la kusawazisha,zikiwa zimesalia dakika 8 kabla ya mchezo kumalizika D. Drogba aliwainua tena mashabiki wa chelsea baadaya kufunga goli la ushindi,na kwa matokeo hayo yameifanya chelsea kuwa na point 68.
kessy58.................................................................................

No comments: