Thursday, 3 April 2008

Arsenal yabanwa mbavu na Liverpool


Arsenal jana imebanwa mbavu na Liverpool baada ya kulazimizwa sare ya goli 1-1 katika kinyang'anyiro cha klabu bingwa ulaya katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa emirate.Arsenal ilikuwa ya kwanza kuchungulia nyavu za liverpool katika dakika 24 baada ya Adebayo kuunganisha kwa kichwa pass ya Van Persie,dakika mbili baadaye Liverpool walisawazisha goli kupitia kwa Dirk Kuijt.Kipindi cha pili kilianza kwa mikiki na katika dakika ya 65 Arsenala walinyimwa penati na mwamuzi baada ya Dirk Kuijt kumshika A.Hleb.Katika kinyang'anyiro kingine cha klabu bingwa ulaya ilizikutanisha timu kati ya Fenerbahce ya uturuki na chelsea ya uingireza.Fenerbahce iliikandamiza chelsea kwa magoli 2-1.Marudiano ya mechi hizo yatafanyika tarehe 09/04/08.
kessy58...........................................................................

No comments: