Wednesday 27 May 2009

Klabu bingwa ulaya leo,Barcelona na Manchester United.







LEO ndiyo leo. Baada ya kelele, majigambo na tambo za kila aina Barcelona ya Hispania na Manchester United ya Uingereza, zinaumana usiku huu katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.Mechi hiyo inayokutanisha mafahari wawili na timu maarufu duniani itapigwa kuanzia saa 2:45, usiku kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini hapa.Katika mechi hiyo, Man United inapigania kutwaa kombe hilo kwa mara ya nne na pia ikitaka kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza Ulaya kutetea taji hilo.Barceloma 'Barca' wao wanataka kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu angalau kupunguza tofauti yao na wapinzani wao wa jadi, Real Madrid ya Hispania iliyotwaa kombe hilo mara tisa.Klabu zingine zilizotwaa kombe hilo mara nyingi ni Liverpool ya Uingereza na AC Milan ya Italia mara 5 kila moja.United "Mashetani Wekundu" wanakutana na Barcelona fainali ya kwanza katika historia ya klabu hizo maarufu duniani.Zote zinaingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu zilizo sawa kwa kila moja kutwaa ubingwa katika Ligi Kuu ya nchi yake msimu huu unaomalizika. Barcelona iliingia fainali kwa kunufaika na goli la ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Chelsea ya Uingereza katika mchezo wa marudiano jijini London baada ya kutoka suluhu mechi ya awali Barcelona.Kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson ambaye anapigania taji la 26 katika misimu 23 ya kuwaongoza Mashetani Wekundu anasema kwamba pambano hilo litakuwa la kuvutia."Uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili wanaonesha ni kiwango gani cha mpira kitaoneshwa," alisema Ferguson.Lakini, Ferguson atakuwa na kazi nzito ya kuwaandaa mabeki wke kuikabili safu kali ya ushambuliaji ya Barca ya Thierry Henry, Lionel Messi na Samuel Eto”o ambayo msimu huu imefunga magoli 100.Lakini naye Ferguson ana safu nzuri ya ushambuliaji inayoundwa na Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney, Dimitar Berbatov na Carlos Tevez.
kessy58............................................................



No comments: