Wednesday, 20 February 2008

Arsenal V AC milan,Lyon V Manchester United



KINYANG'ANYIRO cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kinaendelea tena leo, baada ya jana miamba nane kuvaana katika mechi za kwanza kuwania kufuzu robo fainali. Vinara wa Ligi ya Uingereza Arsenal watakuwa nyumbani katika uwanja wa Emirates kuwakaribisha mabingwa watetezi AC Milan ya Italia. Mechi hiyo inakutanisha timu zilizo katika nafasi tofauti katika Ligi zao za nyumbani, Arsenal inaongoza kwa tofauti ya pointi tano wakiwa na pointi 63 mbele ya Manchester United ambayo mwishoni mwa wiki iliwafunga mabao 4-0 katika mechi ya kuwania kombe la FA. Milan ambayo pia ni klabu bingwa ya dunia iko katika nafasi ya tano inapitwa na Inter kwa pointi 21 katika ligi ya Serie A inakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi. Arsenal itataka kuwafurahisha mashabiki wake baada ya kusononeshwa na kipigo cha United cha mabao 4-0. Mechi nyingine za leo Barcelona itapambana na Celtic mjini Glasglow Skotilandi na Manchester United itakuwa ugenini Ufaransa kuchuana na Lyon, huku Fenerbahce itakuwa nyumbani Uturuki kuchuana na Sevilla.
kessy58.......................................................

No comments: