Tuesday, 4 March 2008

kitimutimu ulaya leo


TIMU nane zitakazofuzu hatua ya robo fainali kutoka timu 16 zitaanza kujulikana leo na kesho, ambapo miamba hiyo itapambana katika viwanja tofauti.
Katika hatua ya mtoano ya timu 16, Uingereza imeingiza timu zake zote nne kubwa Arsenal, Manchester United, Chelsea na Livepool. Arsenal leo itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa San Siro kuchuana na mabingwa watetezi AC Milan, ambapo italazimika kushinda, ili kusonga mbele, baada ya kutoka suluhu katika mechi ya awali iliyofanyika Uwanja wa Emirates wiki mbili zilizopita.
Kama Arsenal itashinda itakuwa ni timu ya kwanza kuifunga Milan kwenye uwanja wao, lakini Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumini ya kuvuka kama walivyofanya mwaka 2003 kwa kuilaza Internazionale mabao 5-1 katika uwanja wa San Siro katika ligi hiyo.
Katika mechi nyingine kesho Liverpool nayo itakuwa ugenini nchini Italia kupambana mabingwa wa nchi hiyo Inter Milan, huku ikitakiwa kulinda ushindi wake wa mabao 2-0 ilioupata katika mechi ya awali katika uwanja wao wa Anfield.
Manchester United itaikaribisha Lyon ya Ufaransa katika Uwanja wa Old Trafford, huku ikipewa nafasi ya kubwa ya kusonga mbele baada ya kutoka bao 1-1 katika mechi ya awali Ufaransa.
Manchester inaonekana kuwa katika kiwango kizuri kwani katika mechi zao nne zilipita wamefunga magoli 13, ambapo katika mechi ya ligi dhidi ya Fulham kocha Alex Ferguson aliwapumzisha baadhi washambuliaji, akiwemo Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo pengine kwa ajili ya mechi ya leo. Matokeo ya sare ya aina yoyote au ushindi utaivusha United.
Mechi nyingine leo itaikutanisha Barcelona itakayoikaribisha nyumbani Celtic ya Skotilandi. Sevilla ya Hispania itaikaribisha nyumbani Fenerbahce ya Uturuki huku ikikumbuka kipigo ilichopata katika mechi ya awali kwa kufungwa mabao 3-2, ili kusonga mbele itahitajika kushinda hata bao 1-0.

kessy58................................................................................................

No comments: