Thursday 12 March 2009

Arsenal yatinga robo fainali,Jose Mourihno alizwa na Ferguson




Timu ya Arsenal imetinga robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa ulaya baada kuinyuka AC-Roma toka Italy kwa magoli 7-6 yaliyopatikana kwa njia ya penati.Nao mabingwa watetezi kwa kombe hilo Manchester united imeifunga bila huruma timu ya Inter toka Italy kwa magoli 2-0,goli la kwanza na Manchester lilifungwa na N. Vidic katika dakika ya nne ya mchezo na pili lilifungwa na C. Ronaldo katika dakika ya 49.Katika mtanange mwingine wa mashindano hayo timu ya Barcelona imesonga mbele katika mashindano hayo kwa kuicharanga timu ya Lyon toka ufaransa kwa magoli 5-2.FC-Porto toka ureno imesonga mbele baada ya kutoka suluhu ya magoli 2-2 katika mechi yao ya kwanza na ya pili wametoka suluhu ya bila kufungana.
kessy58.......................................................


No comments: